Mashetani Wekundu wa Manchester United wametangaza kikosi chao kamili kwa ajili ya mapambano ya michuano mikubwa sana huko barani Ulaya, Champions League ya UEFA.
Kwenye orodha ya majina hayo hakuna mlinzi wa klabu hiyo, Matheo Darmian ambaye alisemekana kwamba ataondoka klabuni hapo wakati wa dirisha lililopita la usajili majuu ambapo tangu msimu huu wa EPL uanze Darmian alicheza mchezo wa kwanza tu wa Man United vs Leicester ambapo alicheza muda wa dakika zote 90 ila baada ya hapo hakucheza tena!
Mbadala wake?
Badala yake sasa klabu ya Man United imemtaja mchezaji Diogo Dalot kwenye kikosi hicho. Huyu Diogo alisajiliwa na klabu ya Man United wakati wa dirisha lililopita la usajili kutokea FC Porto ambapo inaonekana kwamba mwisho wa Darmian kuitumikia United umekaribia!
Naye Marcus Rashford pia hayumo kwenye orodha ya wachezaji wa Manchester United walioorodheshwa kwa ajili ya kuanza mbio za Champions League ambapo yeye inatokana na umri wake kwani kwa sheria za Champions League mchezaji ambaye amezaliwa tarehe 17 Januari, 1997 au baada ya hapo huwa anaweza kuchezea timu yake katika michuano hiyo hata kama jina lake halipo kwenye orodha A ya majina yaliyowasilishwa UEFA!
Oktoba 19 mwaka huu klabu ya Man United itaanza hekaheka zake za kuwinda ubingwa wa Champions League na watamenyana na New Boys kabla ya kwenda kukutana na Valencia ya Hispania. Tangu mwaka 2011, Manchester United hawajawahi kupenya kwenye robo fainali.
Kikosi kamili cha Man United:
Makipa: David De Gea, Lee Grant, Sergio Romero
Walinzi: Victor Lindelof, Eric Bailly, Phil Jones, Chris Smalling, Marcos Rojo, Diogo Dalot, Luke Shaw, Antonio Valencia, Matteo Darmian
Viungo: Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Andreas Pereira, Fred, Ashley Young, Ander Herrera, Marouane Fellaini, Nemanja Matic, Scott McTominay
Mafowadi: Alexis Sanchez, Romelu Lukaku, Anthony Martial.


Povel
Habar njema
Issa
Habari njema