Wakala wa Hector Herrera, bwana Gabriel Moraes anasema kuwa staa huyu hataondoka Porto mwezi Januari.
Mkataba wake ulikuwa unaisha mwaka 2019, yupo katika orodha ya mastaa ambao watakuwa wachezaji wachezaji huru mwakani.
Kuisha kwa mkataba wa Herrera kumewaweka macho klabu za Inter na Roma ambao wanahusishwa kumuhitaji mkali huyu. Jicho la Liverpool pia lilimtamani staa huyu wa Porto.
Wakala anasema, “hawezi kuondoka Porto msimu huu, anataka kuheshimu mkataba hadi utakavyoisha.”
Wakala huyo anasisitiza kuwa kumekuwa na mazungumzo kadhaa lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufikia makubaliano na Porto pamoja na Herrera mwenyewe.
Kwa sasa staa huyu anawekeza jitihada zake katika msimu huu, anaheshimu maamuzi ya timu yake na ni kapteni. Wakala anasema wanao mda mrefu hadi kufikia Januari, na yeye kazi yake ni kuweka sawa mambo kujua hatma ya staa huyu.


Povel
Herera mchezaj mzuri sana