Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegu amekosoa mpango wa kucheza gemu ya La Liga nchini marekani akidai unapoteza ushindani unaotakiwa.
Jumanne Barcelona, Girona na La Liga waliomba ruhusa kwa Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) kuwa klabu hizo zibadilishiwe gemu yao wachezee Marekani.
Gemu ya Girona kama mwenyeji inategemewa kufanyika Miami Hards Rock Januari 26. Kocha huyo anasema hajapenda kabisa mfumo huo kwa kuwa unaathiri ushindani katika ligi.
Kocha huyu anaona ili kuwe na ushindani katika ligi basi timu zote ni vyema zikacheza kwa kutumia viwanja vilevile kwa wote, hii italeta usawa wa kiushindani.
Shirikisho la Soka la Uhispania, Shirikisho la soka Marekani, UEFA, Shirikisho la Soka Amerika Kaskazini, na Uongozi wa masuala ya michezo Amerika Kaskazini wanahitajika kupitisha suala hili.
Umoja wa Wachezaji wa Uhispania (AFE) nao wamepinga mechi hiyo baada ya mkutano na La Liga Jumatatu, Lakini inasemekana wachezaji ndio watakaokuwa wasemaji wa mwisho.


Povel
Gud news