Kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1959, timu ya taifa ya Italia wanamaliza mwaka bila kushinda gemu yeyote ya ushindani.
Ushindi wa mwisho wa timu ya taifa ya Italia ulikuwa mwaka jana Oktoba 9 wakiwa wageni wa Albania katika mechi za kufuzu Fainali za kombe la Dunia.
Kwa sababu Italia gemu yao nyingine ya kimataifa itakuwa baada ya Oktoba 9, mwaka huu ni sawa kusema wamemaliza mwaka bila ushindi wa gemu yeyote ya ushindani.
Mechi za kirafiki hazijahesabiwa. Kama mechi za kirafiki zikihesabiwa basi walishinda gemu moja tu dhidi ya Saudi Arabia Mei 28. Zaidi ya hapo wamekutana na vichapo mara mbili na kutoa sare mara mbili.


Furahav
Italia hawako vizuri sana.