Klabu ya Juventus wametangaza hasara ya paundi milioni 19 kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 baada ya kushuka kwa mapato kwa kiasi cha Paundi milioni 58.
Ilitarajiwa kuwa klabu hiyo ingetangaza hasara baada ya Exor-kampuni yenye umiliki, kupitia taarifa zao za fedha kwa mwaka 2017/2018.
Bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo imetangaza leo kuwa mwaka wa fedha 2017/2018 umefungwa kwa hasara ya paundi milioni 19.2, ikiwa ni ongezeko hasi la paundi milioni 61.8 ukifananisha na faida ya paundi milioni 42.6 ya mwaka uliopita.
Sababu kubwa iliyotajwa kupelekea hasara hiyo ni kushuka kwa mapato, na pia matatizo yanayohusiana na mapato na matumizi kwa kwa wachezaji na rasilimali nyingine za kuendesha klabu hiyo. Juventus pia wanatajwa deni lao kukua kutoka paundi milioni 147.3 hadi kufikia paundi milioni 309.8.
Povel tz
Duh majanga