Timu ya Beckham Inamvizia Messi

Taarifa zinadai kuwa staa wa zamani wa soka, David Bekham anamtazamia staa wa Barcelona Lionel Messi kwa ajili ya timu yake mpya Inter Miami inapokwenda kuanza rasmi kucheza katik ligi mwaka 2020.

Inter Miami inatajwa kuwa klabu ambayo inaweza ikawavutia mastaa wengi kufuatia kujulikana kwa David Beckham akiwa nyota aliyetamba sana enzi zake anacheza soka.

Mkataba wa Messi Barca unaisha msimu wa mwaka 2020-2021, wakati huo bingwa huyu atakuwa anafikia umri wa miaka 33. Kwa mujibu wa Daily Mail chanzo cha karibu na Bekham kimedai kuwa hakuna mawasiliano waliyofanya na Messi lakini anakubali kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumpata mkali huyo.

Nyota huyu wa Barca aliripotiwa kuwa anatazamia kumaliza kuichezea timu yake ya Barca  baada ya kuisha mkataba wake na haitarajiwi kama atakwenda timu yeyote kubwa Ulaya kama akiamua kuendelea na soka.

Kwenda Miami kunadaiwa kuwa sehemu ambayo Messi atakuwa huru zaidi yeye na familia yake huenda akaamua kwenda huko na akakacha kwenda Argentina.

2 Komentara

    Ni safi ikijiunga

    Jibu

    Itakuwa vizuri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.