Maurizio Sarri Avunja Historia!

Boss wa Chelsea Maurizio Sarri ameingia katika historia kwa kuwa kuwa mmoja kati ya makocha 4 katika Premier League kushinda gemu zake tano za mwanzo, Pia amekuwa muitalia wa pili baada ya Carlo Anzelloti.

Muitalia huyu aliingia chelsea baada ya mvutano wa hapa na pale na Napoli, na sasa ameanza kuonyesha kwa nini wakubwa wa Stamford Bridge walikuwa hawana namna zaidi ya kumchukua mkali huyu.

Sarri ni kama ameipatia Premier league, anaweza kujivunia kwa kikosi chake kuanza vyema kabisa ligi hii kwa ushindi wa gemu zote tano, Hii inafanya Chelsea waendelee kuwa na mwanzo mzuri wa michuano hii tangia mwaka 2010.

Lakini Pia, Meneja huyu ameingia katika kitabu cha historia kama mmoja wa makocha wa 4 tu ambao wamefanikiwa kuanza vyema michuano ya ligi hii kwa kushinda gemu tano.

Ancelotti aliwahi kufanya hivyo chelsea mwaka 2010, Pep Guardiola alifanikiwa kufanya hivyo Man City na Craig Shakespeare alipata mafanikio yanayofanana na hayo mwaka 2017 pale Leicester City.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.