Floyd Mayweather amesema anarudi ulingoni kuzichapa na Manny Pacquiao. Mabondia hawa walichapana mwaka 2015 mwezi Mei huku Mayweather akishinda kwa kumzidi pointi Pacquiao.
Mayweather alitangaza kustaafu akidai hataingiua tena tena ulingoni labda kuwe na dau nono zaidi. Sasa Mayweather ametangaza kurudi tena ulingoni.
Kupitia picha ya video inayosambaa katika mitandao mbalimbali bondia huyu amesikika akisema anatoka kwenye ustaafu wake na kuingia kupambana tena na mpinzani wake wa mwaka 2015.
Pambano la mwisho la bondia huyu ilikuwa mwaka 2017 akizichapa na McGregor, pambano hili lilimuendesha hadi raundi ya 10 alipofanikiwa kumchapa kwa KO. Baada ya hapo alitangaza kustaafu na sasa anataka kurejea, Kunani? au ni dau tamu kama alivyodai ndio liingemrudisha ulingoni!


Ester jackson
Namkubali sana my wreather
Povel
Bonge la pambano hlo
Issa
Mayweather ngumi jiwe
Fatina mfingi
Ilo pambano litakuwa powah sanaa!!