Meneja wa Man City Pep Guardiola anadai dau alilolitaja kwa mchezaji Kelvin De Bruyne lilikuwa ni janja janja ya kusema mchezaji huyo hayupo sokoni kwa sasa. Amesema haya kuondoa mkanganyiko katika dau alilolitaja mwanzo.
Mkataba alionao kwa sasa unadaiwa kuwa ni wa thamani ya paundi milioni 223. Lakini mwanzoni meneja huyu aliripotiwa akisema kuwa hakuana sheria ya kumzuia mchezaji huyo huku akidai kuwa kwa klabu itakayomuhitaji italazimika kulipa paundi milioni 250.
Baada ya maneno maneno Guardiola amerejea kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ile haikua thamani ya mchezaji huyo lakini ilikuwa ni namna ya kusema kuwa mchazaji huyo hauzwi.
Staa huyu sasa yuko mbioni kurejea uwanjani baada ya kusumbuliwa na goti toka mwezi Agosti.


Asha mvugalo
Gurdiola ni kocha mjuzi sana