Jadon Sancho amesajiliwa na United baada ya mbio za muda mrefu timu hii kuwania saini ya mwamba huyu, lakini bado suala la atavaa jezi namba ngapi bado ni kizunguzungu kisicho na majibu.
Taarifa rasmi kutoka Manchester zinadai kuwa shati nyingi za Sancho zilizo na namba saba zimeuzika sana siku za usoni lakini bado haijatangazwa kama ni kweli mchezaji huyo atavaa namba hiyo.
Jadon alipokuwa Dortmund alikuwa akivaa namba saba lakini pale United namba saba inavaliwa na Edson Cavani na haitokuwa busara sana kumnyang’anya jezi hiyo nguli huyo wa soka.
Kwa upande wa Solskjaer, yeye anadai kuwa bado baadhi ya karatasi kumaliziwa kusainiwa ili waweze kumtangaza mchezaji huyo. Licha ya Sancho, United wapo njiani kunyaka saini ya beki wa Madrid, Rafael Varane.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Sarah
Asante kwa taarifa