Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba ananyatiwa na Paris St-Germain msimu huu wa joto na klabu hiyo ya Ligue 1 inapanga kuuwauza wachezaji kadhaa kukusanya £50m wanazoamini zitafanikisha azma ya kumpata Pogba.
Tetesi zinasema, Barcelona wanajikakamua kuuza wachezaji ili kufadhili mkataba wa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, kabla ya msimu mpya kuanza.
Mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 28, ana matumaini uhamisho wake kwenda Manchester United utakamilishwa siku chache zijazo.

Ajenti wa kiungo wa kati wa Juventus Mtaliano Nicolo Fagioli, 20 – ambaye ni sehemu ya mkataba wa kubadilishana mchezaji wa Sassuolo Manuel Locatelli – amethibitisha kuwa mahasimu wao Arsenal wamewasilisha dau la £34m kumnunua.
Arsenal wako tayari kuipatia Leicester City wachezaji kadhaa – akiwemo winga Muingereza Reiss Nelson, 21 kama sehemu ya mkataba wa kumsaini kiungo wa kati wa England James Maddison, 24.
Tetesi zinasema, Chelsea huenda wakawasilisha dau la £135m kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20.
Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano na winga wa Sevilla Mhispania Bryan Gil ambao utamwezesha mshambuliaji wa Argentina Erik Lamela kuhamia klabu hiyo ya La Liga club.

Juventus wanatathmini uwezekano wa mkataba wa kubadilishana wachezaji ambao utamwezesha Cristiano Ronaldo, 36, kujiunga na PSG nao wampate tena mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 28.
Tetesi zinasema, Juventus wameweka £35m kuwa bei ya kumuuza mlinzi wa Mturuki Merih Demiral, ambaye anahusishwa na uhamisho wa kwenda Everton.
Tetesi zinasema, Leeds United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Lewis Bate,18.
Tetesi zinasema, Winga wa Bayer Leverkusen Demarai Gray,25, alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu siku ya Jumanne anapokaribia kusajiliwa na Everton.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Sarah
Ziko bomba