Makamu wa rais wa Klabu ya Juventus, Pavel Nedved amedhibitisha mshambuliaji wao, Cristiano Ronaldo atasalia katika klabu hiyo msimu huu.

Ronaldo amehusishwa na kuondoka kwa miamba ya Serie A msimu huu wa joto baada ya kampeni ya mbaya za msimu wa 2020-21.
Paris Saint-Germain inasemekana inavutiwa kumsajili nyota huyo wa Ureno, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Nedved, hata hivyo, anasema mchezaji huyo wa miaka 36 haendi popote na atarudi kutoka likizo yake ya kiangazi mwanzoni mwa wiki ijayo.
Aliiambia Sky Sport baada ya ushindi katika mechi ya kirafiki wa 3-1 wa Bianconeri dhidi ya Cesena: “Ronaldo ameitwa kikosini Julai 26, atarudi Jumatatu na atakaa nasi.”
Ronaldo alijiunga na Juventus akitokea Real Madrid mnamo 2018. Amefunga mabao 81 katika mechi 97 kwenye Serie A tangu kuwasili kwake.
Licha ya kiwango kibovu cha Juventus msimu uliopita, alimaliza msimu kama mfungaji bora wa Serie A na mabao 29 katika michezo 33.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Sina uhakika sana na CR7 kuendelea kusalia Juventus, Subiri tuone
Sarah
Jambo zuri