Meneja wa Ukraine, Andriy Shevchenko amemaliza mkataba wake kama meneja wa Ukraine, wiki chache baada ya kuiongoza nchi yake kwenye robo fainali ya Euro 2020.

Shevchenko aliteuliwa kuwa meneja wa timu ya Ukraine mnamo Julai 2016 na ameiongoza jumla ya michezo 52, pamoja na michezo mitano kwenye Euro za msimu huu wa joto.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan na Chelsea alitangaza kuondoka kwake kupitia kurasa yake ya Instagram, hapo jana.
“Nimetumia miaka mitano na timu ya taifa,” Shevchenko aliandika kwenye Instagram.
“Kwa bidii tumeonyesha kuwa tuna uwezo wa kucheza mtindo wa kisasa wa mpira wa miguu.
“Asante kwa mashabiki wote kwa msaada wenu na ukosoaji. Tumeonyesha pamoja kwamba tunaweza kuwa na ushindani na kufurahi.”
Shevchenko, ambaye alicheza mechi 111 kwa Ukraine, akifunga mabao 48 kati ya 1995-2012, alichezea klabu yake ya nyumbani ya Dynamo Kiev ambapo alishinda mataji matano ya ligi ya Ukraine kabla ya kujiunga na AC Milan kisha Chelsea.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Mapumziko mema Shenko