Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha kuwa pendekezo la Granit Xhaka kuhamia Roma haliwezekani na anaamini kiungo huyo kuwa ni mchezaji muhimu wa timu hiyo msimu huu.

Mapema msimu wa joto, kiungo huyo alionekana kuwa na uhusiano wa karibu na Jose Mourinho katika klabu ya Serie A, ingawa wiki iliyopita ripoti zilianza kusambaa kwamba Xhaka atabaki na Gunners.
Xhaka hivi karibuni alirudi mazoezini kabla ya kuichezea Arsenal katika mechi ya kirafiki ambayo walipoteza mabao 2-1 dhidi ya Chelsea jana [Jumapili], na maoni ya Arteta yakikuja baada ya mechi hiyo.
“Granit [Xhaka] atabaki nasi. Ni mchezaji muhimu katika kikosi chetu, ” Arteta alithibitisha.
Xhaka alifanikiwa kusawazisha goli kwa kichwa baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Nicolas Pepe katika mchezo wa jana waliopoteza dhidi ya Chelsea.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Habari njema