Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemuunga mkono Anthony Martial kudhibitisha mashaka yake kuwa na makosa na anaamini mashabiki wataona mchezaji tofauti na yule wa msimu uliopita.

Solskjaer alikanusha kwamba mshambuliaji huyo anaweza kuondoka klabuni kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho mwishoni mwa mwezi na kuelezea ni kwanini ana matumaini msimu huu utakuwa tofauti kwa Martial.
Solskjaer aliulizwa katika mkutano wake wa waandishi wa habari dhidi ya Leeds ikiwa anafikiria Martial ana kile kinachohitajika kuwa No 9 wa Man Utd.
Alijibu: “Kama nilivyosema kabla tunajua uwezo wa Anthony. Msimu uliopita ulikuwa wa mbaya, tulikuwa na majeraha, alipoteza fomu, msimu kabla ya kuwa mfungaji bora wetu.
“Kama Anthony atapiga penati zote, au Marcus Rashford angepiga penati zote msimu uliopita, hayo ni magoli mengine 10-15 kwa mshambuliaji wa kati lakini tuna Bruno [Fernandes] ambaye anajiamini sana kwenye penati huwezi kumzuia kwakweli.
“Ninajiamini sana na ninapenda kile ninachokiona kutoka kwa Anthony ninapomuona kwenye mazoezi sasa, na wakati ninamwona kwenye gym ana kitu kipya zaidi sasa.”
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!



Sania+mapua
Ngoja tuone
Sarah
Vizuri