Baada ya Simba na Yanga kutangaza kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao nchini Morocco, wababe wenzao Azam wamewakwepa na kupanga kupiga kambi nchini Zambia katika jiji la Ndola.

Azam walikuwa na mapendekezo mawili ya kambi ambapo walipanga kwenda nchi moja kati ya Afrika Kusini na Zambia hatimaye huenda siku za hivi karibuni wakasafiri kwenda Zambia sehemu ambayo aliipendekeza kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina.
Maandalizi hayo yamepangwa kuanza wiki ijayo kama mambo yataenda vizuri na timu tayari ipo kambini Chamazi, ikijifua tangu Jumatatu ya wiki hii ikisubiri taratibu za kwenda Zambia zikamilike.
Moja ya vigogo wa Azam amesema kuwa wamefunga hesabu kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa na sasa wako kwenye harakati za kunasa nyota wasiozidi watatu wa ndani kisha kwenda Zambia.
“Usajili wa wachezaji wa kigeni tumemaliza, tumebakiza nafasi chache tu za wachezaji wa ndani ambao kwa sasa siwezi kuwataja,” alisema.
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!



Sania+mapua
Azam kibarua wanacho