Kutoka UFC Mpaka Soka, Khabib Asaini na Legion Dynamo

Baada ya kutundika grovu za UFC, Khabib Nurmagomedov amesema kwamba atakuwa wazi kucheza soka la kulipwa.

Kutoka UFC Mpaka Soka, Khabib Asaini na Legion Dynamo

Na kwamujibu wa RT ndoto zake zimetimia baada ya kusaini dili na Legion Dynamo, ambayo imeanzishwa mwaka 2015.

Khabib ni rafiki mzuri wa Christiano Ronaldo, na mara nyingi amekuwa akisema kwamba anapenda kutazama mpira na MMA.

Bondia huyo wa zamani na bingwa wa UFC katika uzito wa kati mwezi Januari alionesha ujuzi wake kwenye mechi huko Dubai dhidi ya mkongwe wa AC Milan Clarence Seedorf.

Khabib kwenye mwezi huo aliweka video iliyokimbiza huko Instagram akiwa ameweka ujumbe uliyosomeka: “Nikijiandaa kwaajili ya mchezo wangu wa kwanza katika soka, mimi ni mchezaji huru na nipo tayari kupokea ofa.

Kutoka UFC Mpaka Soka, Khabib Asaini na Legion Dynamo

Kisha akapata ofa kutoka kwa klabu ya Urusi inayojulikana kama FC Kamaz, ambao walikuwa tayari kumfanyia majaribio staa huyo wa MMA.

Haijajulikana ni lini staa huyo wa miaka 32 ataanza kufanya kazi kwenye upande wake mwingine wa kipaji na alicho thibitisha ni kwamba hatoweza kurejea tena kwenye UFC.

Ngoja tuone kama Khabib ataweza kung’aa kwenye soka kama alivyong’aa kwenye ndondi.


SHINDA NA TIKI REWARD KASINO

Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!

Tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Khabib yupo vizur

    Jibu

    Khabib mtu makini

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.