Klabu ya Barcelona wametangaza kuwasajili katika ligi kuu ya hispania (Laliga) mchezaji, Memphis Depay, Eric Garcia na Rey Manaj baada ya kufikia makubaliano na Gerard Pique kupunguza mshahara wake.
Barcelona walikuwa wamefikia 95% ya mishahara yote ilikuwa haiwezekani kuweka sajili zao mpya kama Memphis Depay na Eric Garcia kutokana na kupitiliza asilimia zilizowekwa na La Liga.
Ililazimika mchezaji mmoja anaelipwa pesa kubwa ajitolee kukatwa sehemu kubwa ya mshahara wake ili nyota hao waorodheshwe kwenye mfumo.
Gerrard Pique alitoa ushirikiano mkubwa, amekubali kukatwa sehemu kubwa sana ya mshahara wake kufanikisha zoezi hilo.
Licha ya watu wa kambi ya Pique kukataa zoezi hilo ila yalikuwa maamuzi yake binafsi kwa mapenzi yake kwa Klabu.
Barcelona wamedhibitisha wachezaji wote watatu waliosajiliwa watakua katika kikosi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Real Sociedad utakao pigwa leo.
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!



Sania+mapua
Pique ameonyesha mapenzi ya kweli kwa Barcelona