Shabiki namba moja wa Arsenal na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame ameonyesha kusikitishwa kwake baada ya timu yake ya Gunners kupokea kichapo na timu iliyopanda daraja katika mechi ya kwanza ya msimu.

Brentford, iliyorejea katika ligi hiyo baada ya miaka 74 iliinyoosha Arsenal mabao 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Brentford Community Stadium.
Kagame licha ya kuwa shabiki mkubwa wa Arsenal lakini pia serikali yake ilitoa ufadhili wa kutangaza nchi ya Rwanda katika jezi ya klabu hiyo yenye maandishi “VISIT RWANDA”.
Tangu mwaka 2018, serikali ya Rwanda imekuwa na makubaliano ya udhamini wa thamani ya zaidi ya pauni milioni 30 ($ 42m), ambayo inajumuisha nembo ya “Tembelea Rwanda” inaoonyeshwa kwenye mikono ya fulana ya Arsenal.
Baada ya mechi hiyo aliandika katika mtandao wake wa Twitter: “Hatupaswi tu kutoa udhuru au Kukubali upuuzi. Timu lazima iiundwe kwa lengo la kushinda kushinda na kushinda.”
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!



Sania+mapua
Pole kwa wana Arsenal