Usain Bolt mshindi mshindi mara nane wa mishindano ya olympic asema “nimechelewa” kurudi japo anakubali kuwa anapata hamu ya kurudi tena kwenye mashindano.
Mjamaika huyo mwenye miaka 35 nyota yake ilianzaa kuonekana mwaka 2017. Anasema alishawishika tena kurudi katika michezo iliyofanyika Tokyo japo kocha wake nae alimfuata kumshawishi.
“Nimechelewa, kama ningehitaji kurudi basi ingekuwa ni kwenye mashindano ya olympic hii” alimwambia mwandishi wa BBC.

“Nilipomwambia mkufunzi wangu kuwa nataka kustaafu alinikalisha chini na kuniuliza lini unataka kustaafu. Sifanyi chochote kurudi, hakuna. Aliniambia ‘hakikisha uko tayari kwa ajiri ya kustaafu.”
“Kama sio mkufunzi wangu, sitafanya, sababu namuamini na kama akisema hapana basi ni hapana japo napata hamu ya kurudi tena.”
Mbali na kuwa mwanariadha pia ni shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na klabu ya Manchester United.
Baada ya kuikacha riadha, Usain Bolt akahamia kwenye mpira wa miguu na kupita kwenye vilabu kama Valleta fc ya nchini malta na Mariners ya nchini australia huko alidumu kwa wiki 8 tu na akaamua kuachana na michezo.
Usain Bolt kwa sasa anajihusisha na mziki huku akiacha vibao kadhaa ambavyo ameshairikisha wasanii wakubwa wa jamaika kama Christopher Martin, Dexta daps na Ding Dong.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


