Tetesi zinasema, Real Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, ikiwa watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland,21, kutoka Borussia Dortmund msimu ujao.
Tetesi zinasema, PSG wanataka kumsajili mlinzi wa Ujerumani, Antonio Rudiger, 28 ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika majira ya kiangazi.
Manchester United wanamfwatilia mchezaji wa kimataifa wa England na West Ham Declan Rice, 22, kama chaguo lao la kwanza dirisha la uhamisho litakapofunguliwa majira ijayo ya kiangazi.

Real Madrid na klabu kadhaa za Ligi ya Primia zinamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Fulham Fabio Carvalho, 19. Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ureno, ana chini ya mwaka mmoja katika mkataba wake kabla ya kuondoka uwanja wa Craven Cottage.
Borussia Dortmund wamekubaliana juu ya mkataba mpya na kiungo wa kati England Jude Bellingham,18, na hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo msimu ujao licha ya kwamba ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia.
Barcelona italazimika kuilipa Liverpool kima cha euro milioni 20 (£17.1m) kama marupurupu ya ziada ikiwa mchezaji wake Philippe Coutinho, 29, endapo ataichezea zaidi ya mara 100 klabu hiyo ya La Liga.

Tetesi zinasema, Franck Kessie huenda akaondoka AC Milan mwezi Januari mwakani baada ya kiungo huyo wa Ivory Coast aliye na miaka 24, kukataa ofa ya mkataba wa thamani ya euro milioni 6.5 kwa mwaka.
Tetesi zinasema, Mlinzi wa zamani wa Arsenal David Luiz, 34, anapania kurejea nyumbani kwao Brazil baada ya kukataa ombi la kujiunga na klabu ya Marseille.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Arsenal, Mesut Ozil, 32, ananyatiwa na klabu kadhaa za MLS na Qatar baada ya mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Ujerumani kumalizika Fenerbahce.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


