CAF : Simba, Azam, Biashara Waruhusiwa Mashabiki.

 

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kupitia TFF, limeruhusu idadi ya mashabiki 15,000 kuhudhuria mchezo wa Simba SC wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa utakaopigwa Oktoba 24 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Simba SC : Wachezaji Majeruhi Warejea, Kujiandaa dhidi ya Galaxy.

Shirikisho hilo limeweka utaratibu wa kuruhusu idadi ndogo au kuzuia kabisa mashabiki kuingia uwanjani kutokana na kudhibiti kusambaa homa ya virusi vya Corona. Mara zote imekuwa ikisisitiza taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa corona kufuatwa viwanjani.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki kwenye michezo ya kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika kwa timu za Tanzania.

“Kwa mujibu wa taarifa  iliyotumwa leo [jana] Oktoba 14, 2021 mchezo wa Kombe la Shirikisho Biashara United vs Al Ahly Tripoli (Libya) imeruhusu mashabiki 5,000 wakati ule wa Jumamosi Azam FC vs Pyramids FC (Misri) imeruhusu mashabiki 2,000.

“Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Simba SC vs Jwaneng Galaxy (Botswana) CAF imeruhusu mashabiki 15,000.

CAF imesisitiza kuwa kwa mujibu wa utaratibu mechi zote za CAF na FIFA zinatakiwa kuchezwa bila mashabiki kutokana na sababu ya Uviko19 (Covid19) lakini tathmini walioifanya baada ya kupata maombi wameruhusu idadi hiyo ya mashabiki na kuzitaka kalbu kufuata utaratibu, endapo zitakiuka hatua kali zitachukuliwa.” ilisomeka taarifa hiyo kutoka TFF.


PIGA MKWANJA NA LA ROUGE

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.