Raheem Sterling Afungua Milango Kuondoka Etihad

Kumekuwa na maneno mengi kwa siku za hivi karibuni, wengi wakihoji ni ipi nafasi ya Raheem Sterling kwenye kikosi cha Manchester City?

Maswali haya na mengine mengi, yamejitokeza baada ya usajili wa Jack Grealish ambaye amekwenda moja kwa moja kwenye kikosi cha Pep Guardiola akicheza namba ya Sterling tangu msimu huu umeanza.

Uwepo wa Grealish, kuimarika kwa kiwango na nafasi ya Phil Foden, kumemfanya Raheem Sterling kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha City na hivyo amekuwa akisugua benchi kwa muda.

Hakika, hili sio suala ambalo Sterling analifurahia hata kidogo. Ikumbukwe kuwa, huyu ndiye alikua miongoni mwa wachezaji waliokua na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya City hasa msimu uliopita. Kwa hili, Raheem ameamua kuwa wazi hisia zake na ulimwengu utambue.

Grealish, De Bruyne na Foden.

Akizungumza na Financial Times Business of Sport US Summit, Sterling amenukuliwa akisema;

Kama kunauwezekano wa kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kupata muda zaidi wa kucheza, nitakuwa tayari kwa hilo. Kama nilivyosema, soka ni kitu cha muhimu sana kwangu.

Kama mchezaji wa kiingereza, kitu pekee ninachokijua ni EPL. Siku zote nimekuwa nikiwaza, labda siku moja nitakwenda kucheza nje ya nchi. Nione ninawezaje kuendana na changamoto za huko.

Hii ni kauli ambayo inatokea wakati ambapo, Raheem Sterling anahusishwa na FC Barcelona pamoja na AC Milan. Swali ni – Je, Sterling ataondoka Etihad katika ya msimu au atasubir msimu huu uishe?


PIGA MKWANJA NA LA ROUGE

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe