Jamie Carragher ni miongoni mwa wachambuzi wa soka wanaojulikana kwa kuwachochea wachezaji na makocha, safari hii, Ole Gunnar Solskjaer ameamua kumpuuza.
Carragher alikuwa wa kwanza kuinyooshea kidole Man United akimlenga Ole Gunnar Solskjaer. Toka msimu uliopita, Carragher amekuwa akiitaka United kumfukuza Ole na kumpatia timu kocha mwingine ili timu hiyo iweze kubeba mataji.
Kwa lugha nyepesi, Jamie Carragher hamuoni Ole kama mtu sahihi wa kuipatia United taji lolote kwenye ulimwengu wa soka. Carragher anaongeza ndimu kwenye kipindi kigumu wanachokipitia Manchester United. Kupoteza michezo 4 kati ya 7 waliyocheza (kwenye michuano yote), kunaendelea kumuweka Ole kwenye koti kavu.

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atalanta, Ole Gunnar Solskjaer amechukua uamuzi wa kusafisha hali ya hewa. Amempuuza Carragher na wachambuzi wengine wote wanaotumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kushinikiza aondolewe United.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya Atalanta, Ole amesema;
[Anachokisema Jamie Carragher] Hainiathiri kwa chochote. Ninajiamini kwa kuwa klabu inaimani na mimi. Nina uhakika, maoni ya Jamie Carragher hayobadilisha hilo.
Nina misingi na namna yangu ya kuongoza. Kumekuwa na maneno mengi, lakini tunacheza na Liverpool jumapili na Jamie anahangaika na hivi vitu vidogo vidogo.
United itachuana na vigogo wote wa EPL pamoja na michezo mingine ya Uefa ndani ya wiki 6 zijazo. Vijana wa Ole watabadilisha gia angani au wataendelea kupoteza pointi?
Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.


