Lindelorf Aokoa Jahazi…

Baada ya kuwa na mchezo mgumu hapo jana ambao wengi waliona mchezo huo unaweza kuisha kwa Burnley kuondoka na alama zote tatu pale Old Trafford, mambo yakidhihirika wazi kwamba mpira kweli ni dakika 90 ambapo haikuchukua hata sekunde kabla ya mechi kuisha mlinzi anayefanya vizuri na klabu hiyo kwa sasa, Lindelorf akawapa anaglau alama moja mashabiki waliokuwa wamejazana uwanjani hapo kuishangilia timu yao.

Kwa takwimu zisizo rasmi sana klabu ya Burnley mara nyingi amekuwa akiwasumbua wakubwa waligi hiyo japo katika miaka ya karibu amepotea kidogo, kitu ambacho kinampa umaarufu katika ligi hiyo. Hilo linatokana na baadhi ya wachezaji hao kukaa kwa kipindi kirefu pamoja na kuwa na muunganiko mzuri wa muda mrefu.

Mechi kama ile inafananishwa na Manchester wa miaka ya 2006 ambayo kwao kufungwa idadi ike ya magoli haikuwa kitu kwao kwa sababu walikuwa na uwezo wa kusawazisha makosa yao na kuibuka na ushindi tena katika mechi hizo. Hilo linaonekana kuanza kujitokeza tena kwa timu hii iliyopo kwa sasa na uwezo wao wa kurekebisha makosa na kutafuta ushindi tena hata kama walipotea kimchezo.

Ole anaamini kwamba, kilichofanywa na klabu hiyo jana ni jibu halisi la kudhihirisha kwamba klabu hiyo kwa sasa imebadikika na haipo kama ilivyokuwa mwanzo, na kila mmoja analiona hilo kwa aina ya soka wanalocheza kwa kipindi kikichopo, na yeye hajawalaumu kwa kiwango walichokionesha ila amewasifu kwa kuwa na moyo wa upambanaji hadi kupata matokeo kwa wakati ule.

Ole ambaye ameshinda mechi zake zote sita za mwanzo akiwa kama mwalimu wa kikosi hicho ameonesha mabadiliko makubwa kikosini hapo kwa kubadili mfumo mzima uliokuwa unepandikizwa ndani ya klabu hiyo hapo awali. Kocha huyo miongoni mwa vitu vinavyomfanya aonekane anafanya makubwa ni ile hali ya kuwaamini wachezaji anapowapa majukumu kwenda kutafuta alama tatu; pia suala la kuwafanya wachezaji kama sehemu kubwa ya washauri na kuwaruhusu kutunia nafasi zao wanapozipata.

Hadi dakika ya 87 United walikuwa nyuma kwa magoli 2-0 kabla ya mpira wa adhabu uliopigwa na Pogba na kuwarudisha mchezoni; hadi dakika za nyongeza zilivofika Lindelorf alipowapa klabu hiyo zawadi ya goli na kuidhinisha thamani yake kikosini hapo kwa wakati wote.

Jana kocha huyo aliingia akiwa na mfumo tofauti kabisa ya ule uliozoeleka kwa kumuanzisha Pereira ambaye alipotea kabisa kimchezo na makosa yake kuigharimu timu. Pia, aliweza kumpa Lukaku nafasi ya kuwa mshambuliaji anaesimama peke yake akisubiri mipira kutoka kwa Mata na Rashford ambapo ulikuwa ni mfumo wake wa majaribio baada ya klabu hiyo kumkosa Martial ambaye angeweza kusababisha timu icheze kwenye mfumo uliozoeleka wa siku zote.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    good newz

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.