Kutua kwa nyota huyo kunakuwa mwiba kwa wachezaji waliokuwepo kikosini hapo hadi sasa. Kama ilivyokkwisha tokea kwa Morata ambaye amesaini kuwachezea Atletico kwa mkopo kwa kipindi cha miezi 18; sasa inaonekana inaweza ikawa ni zamu ya Giroud ambaye anakipiga ndani ya klabu hiyo ya Chelsea.
Alijiunga na miamba hao akitokea kwa wapinzanibwao na watanibwa muda mrefu klabu ya Arsenal. Lakini naye hajawa na nafasi kubwa sana tangu ajiunge na kikosi hicho kwa kipindi chlte hicho, kuchangia hali hiyo na kutua kwa Higuain inawezekana ikawa ni nafasi yake ya pekee kuachana na klabu hiyo kwa sababu kadri wakati unavoenda mchezaji huyo atazoea ligi na kupata namba ya kudumu na wengine kupoteza nafasi zao.
Nafasi yake ya kuendelea kusalia ni finyu kutokana na takwimu zake kikosini hapo akiwa na idadi ya chini kabisa ya magoli. Amecheza jumla ya mechi 45 na kati ya hizo amefanikiwa kufunga magoli 10 tu. Na katika mechi zote hizo amecheza dakika zote 90 katika mechi moja tu nyingine zote ameanzia benchi; kitu kama hiki hakionekani kama ni furaha kubwa kwake kwa sababu ni mchezaji ambaye ana vigezo na hadhi ya kimataifa na ingefaa apate chapuo kuwa katika kikosi cha kwanza. Na sasa kutokana na uhaba huo wa magoli klabu imeamua kumpeleka Higuain amalize ukame huo.
Mawazo yake ya kutimka hapo hayajaanzia hapo baada ya Higuain kutua bali pia suala la mfumo baada ya kochwa wao kulazimisha Hazard awe mshambukiaji namba tisa kivuli kwenye mechi nyingi zilizochezwa suala hilo linaonekana kuwa ni gumu sana kwake kwa sababu ni dalili za mwanzo kabisa za kupokwa namba yake na kukabidhi kwa mtu mwingine.
Katika umri wake wa miaka 32, Higuain bado ana nafasi ya kufanya makubwa popote atakapopata nafasi kutokana na uwezo wake uwanjani. Hata akifanikiwa kutoka ndani ya klabu hiyo bado anaweza kufanya maajabu makubwa sana. Kwa sababu uwezo wake bado haujapotea tangu pale alipokuwa Arsenal; bado ana ari ya kitoa matokeo na kuleta ngubu kwenye kikosi chochote.
Alifanya makubwa sana upande wa timu ya taofa pamoja na kwamba hakuweza kufunga kwenye michuano ile. Japo uwepo wake ulichagiza nafasi ya timu ile kuchukua ubingwa, hivyo uwezo wake bado yupo sokoni kiasi cha kumfanya ashindwe kusajiliwa anapotaka.Kitendo chake kuondoka ndani ya klabu yangu bado sioni kama kuna sababu; kwa umri wake kuendelea kutokea benchi na isitoshe ana uwezo wa kucheza dakika zote 90 bila kuwa na tatizo lolote na kuonesha kiwango kilekile. Hivyo ni suala linaloweza kumfanya atimke kwa kipindi chochote.


Povel
Gud news