United Kukutana na Sarriball kwenye FA

Katika upangaji wa pacha uliofanyika siku ya jana umeweza kutoa pacha ambazo kila timu itakutana nayo kwenye hatua ya tano ya michuano hiyo. Zikiwemo na klabu nyingine lakini hawa wawili watakutana kupata mmoja atakayesonga mbele kwenye hatua inayofuata ili kuendelea kusonga hatua ya nusu na robo fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Katika hatua hiyo wawili hao pekee ni klabu kubwa zitakazokutana na lazima mmoja atoke ili kupisha nafasi ya mwingine ipatikane aweze kusonga mbele zaidi. Huu kwa sasa ni uwanja wa Man City kufanya maajabu kwenye michuano hiyo kwa sababu kwa uwezo wake na mpinzani aliyepangiwa naye ni vigumu kusema soka ni mchezo wa makosa kwao. Kwa namna moja au nyingine lazima watasonga tu mbele.

Kwenye michuano iliyopita, wakati Mourinho akiwa kocha kwenye michuano hii Man United aliwahi kuchezea kichapo cha goli moja kutoka kwa Chelsea na kuwaacha wakafika hatua nzuri sana kwenye michuano hiyo mikubwa Uingereza. Na Chelsea wao walikuwa chini ya Conte katika wakati huo ambaye aliiongoza vizuri klabu hiyo.

Ikiwa baadhi ya timu kubwa zinazocheza ligi kuu zimetolewa kwenye michuano hiyo, ambazo ni Liverpool, Arsenal ma Tottenham ni vilabu viwili tu vya ligi kuu vilivyo nafasi sita za juu ndivyo vinacheza katika kombe hilo kufuatia kuondolewa kwa wakongwe wengine ambao wangekuwa na nafasi ya kuleta ushindani.

Ratiba ya timu nyingine katika michuano hiyo ni; Manchester City hana wasiwasi na kazi yake ya kusukuma gurudumu kusonga mbele kwani atakutana na aidha Middlesbrough au New Port County katika hatua hiyo kitu ambacho hakimtishi sana kwa aina ya wachezaji na kikosi alichonacho kwa wakati huu.

Doncaster Rovers wao wanategemewa kukutana na Crystal Palace ili kuweza kupata mshindi atakayesonga mbele kujua nafasi yake ya kushinda ili kufungua milango ya kushinda michuano hiyo. Pia, Portsmouth atakipiga na Queens Park Rangers katika hatua hiyo ya kutafuta nafasi ya kuzidi kufungua milango ya kusonga mbele.

AFC Wimbledon wao watakutana na Millwall ambapo wote wawili wameonekana na utimamu wa kutosha baada ya kuwagaragaza wakubwa kwenye michuano hiyo. Ambapo, waliweza kuwapiga West ham na Everton kama walivofuata. Kutokana na hilo kunawapa nafasi ya kukutana tena kwenye raundi ijayo.

Ratiba ya wengine ni Bristol City dhidi ya Shrewsbury Town au Wolves, Swansea City dhidi ya Barnet au Brentfold as well as Brighton and Hove Albion or West brom dhidi ya Derby Country. Hao watapambana kumpata mwenye uwezo wa kusonga mbele zaidi kwenye hatua nyingine.

4 Komentara

    Ngoja tuone nani na nani atapita na kumtoa nje kwenye michuano,maana game zote kali hapo lazma niweke mkeka

    Jibu

    Habar nzur

    Jibu

    Good news 👍

    Jibu

    Noma sana hiiii

    Jibu

Acha ujumbe