£21.5M za PSG Kumnasa Idrisa Gueye

PSG wamekunjua dau la paundi milioni 21.5 kama ofa ya kumnasa nyota wa Everton Idrisa Gueye, lakini bado Everton wanaonekana kuhitaji bunda kubwa zaidi, angalau mara mbili ya dau lao kwa mujibu wa Sky Sports!

Mabingwa hawa wa Ufaransa wanahitaji kutatua shida ya Viungo wakiwa wamekumbwa na seke seke la majeruhi kwenye klabu hiyo huku wakikosa mbadala wa kudumu wa Marco Verratti. Wamemtupia macho nyota huyu, Gueye ambaye kwa sasa yupo kwenye fomu nzuri katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Wakati huo Everton, ambao wanatajwa kutaka dau kubwa zaidi ya ofa iliyopo mezani, wao wapo sokoni wakimwinda mshambuliaji baada ya Cenk Tosun kuwa katika kipindi kigumu. Wakati wakitarajia kumnasa Richalison, inadaiwa kuwa Everton hawataweza kumuachia nyota wao hadi wahakikishw wamepata mbadala wake.

3 Komentara

    Safi sana iyo ni fulsa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.