Wiki ya raundi ya 4 ya FA Cup imewaacha vichwa chini baadhi ya watabe wa Ligi Kuu ya Uingereza wakilazimika kuwa watazamaji tu. Baadhi ya timu bado zinakabiliwa na kibarua kingine kabla ya kujihakikishia kucheza kwenye raundi ya 5 ya timu 16.
Watabe kutoka Ligi ya Uingereza walioshuhudia wakiachwa nje ya kupambania kombe hili ni Arsenal, Tottenham, Everton, Burnley, Newcastle, na Westham. Wapo waliosalia, kama ilivyo kwenye orodha hapa chini;
Timu zinazoingia kwenye droo inayofanyika kuelekea raundi ya tano ya michuano ya FA Cup
| 1 Swansea
2 AFC Wimbledon 3 Shrewsbury au Wolves 4 Millwall 6 Bristol City 7 Derby County 8 Doncaster |
9. Chelsea 10. Watford11. Middlesborough au Newport County12. Manchester City 13. Barnet au Brentford 15 Manchester United 16 Crystal Palace |
Droo ya kuelekea raundi ya 5 inafanywa mshindi mara 2 wa kombe hili Ian Wright na Alex Scott. Raundi ya 5 imepangwa kuanza kurindima kuanzia Ijumaa ya Februari 15 hadi Jumatatu ya Februari 18. Ukiacha zawadi zingine, washindi wanachukua kitita cha paundi 360,000


Povel
Hatua ngumu sana