Marko Arnautovic asaini kuendelea kuwatumikia West ham kwa kipindi kingine pamoja na kupata ofa kubwa ambayo yeye anaiita yenye majaribu makubwa kuweza kutimkia China. Aliweza kuhusishwa kujiunga na klabu mbili za nchini humo kwa kitita kikubwa cha pesa lakini amefanikiwa kukwepa ushawishi huo.
Takribani mwezi mzima alihusishwa kujiunga na ama Shanghai SIPG au Guangzhou Evergrande kwa dau nono kama angekubali kujiunga nao. Lakini amefikia maamzi sahihi ya kuweza kusalia katika klabu yake ya muda mrefu na akaongeza mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo kwa kipindi kingine.
Aliachwa hata nje ya kikosi dhidi ya Bournemouth kukiwa na matumaini makubwa kwamba angeondoka klabuni hapo mapema sana. Pia, aliachwa nje kwenye mechi dhidi ya AFC Wimbledon ambayo alishuhudia timu yake ikipokea kichapo cha haraka kilichowastaajabisha wanasoka wengi duniani.
Arnautovic alithibitisha kusalia katika kikosi hicho kwa kutoa taarifa yake kwenye mtandao wa Instagram akisema “Ndugu zangu mashabiki wa West ham, Naamini sio siri tena, nimekuwa nikihusishwa na kuihama klabu yangu na kwenda kujiunga na klabu za huko China, suala hilo lina ukweli na kiuhalisia ofa zao zilikuwa na majaribu sana kwangu na hata kwa wanafamilia wangu”
Miongoni mwa mambo yanayoweza kuwa yamemfanya aghairi maamzi yake ni kutokana na namna klabu hiyo ilivyomlea yeye, anaona akiwa pale ni zaidi ya nyumbani kwake kutokana na kuthamini nafadi yake na kutambua uwezo wake na mchango wake hivyo ilimpa wakati mgumu kutimka klabuni hapo katika mazingira kama hayo.
Wengi wanaonelea kwamba Pellegrin amefanya ushawishi mkubwa wa mchezaji huyo kusalia klabuni hapo. Pamoja na sababu alizozitoa mchezaji huyo lakini zimechagizwa na nafasi ya kiongozi wa klabu hiyo ambaye hapo nyuma alinukuliwa akisema hatma ya kuondoka mchezaji huyo ipo mikononi mwao kama angeruhusiwa kuondoka au aendelee kutumikia klabu hiyo ilimlea kwa kipindi chote hicho.
Wakati anasaini kandarasi yake aliweza kusema kuwa siku zote anaipenda klabu hiyo na anawapenda mashabiki wa klabu hiyo na hakika anafuraha sana juu ya klabu yake hiyo. Pamoja na yote yaliyotokea wayaache na waweze kuendelea na maisha yao ya awali na kufurahia maisha na klabu yao.
Pamoja na kusalia kwake na kuonesha ukomavu ndani ya klabu hiyo lakini bado hajazima ndoto za klabu hiyo kumsaini mchezaji kutoka Celta Vigo Maxi Gomez ambaye kama atatua klabuni hapo atawafanya kuvunja kibubu kwa usajili wa £43.3M ambao kiuhalisia utakuwa ni wa kihistoria klabuni hapo.


Povel tz
Habar njema