Osaka na Kvitova Walizana

Mchezaji huyo wa tenisi raia wa Japan alishinda taji lake la Australian Open na kumwacha mpinzani wake Petra akitoa machozi baada ya kulikosa tajji hilo katika mazingira ambayo yeye mwenyewe hakuamini. Awali Osaka ndiye aliyenza kutoa machozi baada ya mipira yake yote mitatu ya ushindi kuzuiliwa na mpinzani wake kitu ambacho anadai kilimtisha na kumpa wasiwasi kwani alikuta kama nguvu zake zinapotea bila mafanikio lakini baadae aligeuka ni mwenye furaha baada ya kuanza kupata matokeo aliyokuwa anayahitaji.

Kwa makubwa haya aliyoyafanya ndani ya michuano hiyo na ile ya Melbourne inampa nafasi kubwa ya kupanda katika takwimu za wachezaji bora wa tenisi duniani zinazotarajiwa kupangwa siku ya jumatatu. Amefanya makubwa ambayo yanastahili heshima kwa sasa kwani michuano hiyo ina ushindani wa kipekee sana.

Wakati wa mechi hiyo anasema alikuwa anafikiria juu ya nafasi yake kusonga mbele isitoshe hiyo ni fainali yake ya pili katika mwendelezo wake na ana kila sababu ya kuibuka kidedea katika michuano hiyo; hilo lilimfanya aone hana sababu ya kuachia nafasi kabisa. Kuna wakati akawa anapata hisia za kwamba inawezekana yeye ni bora zaidi ya Petra lakini majibu yake akaona hapana. Hapo akapata nguvu zaidi kumdhihirishia na kuidhihirishia dunia kwamba na yeye ni bora zaidi.

Januari mwaka jana Osaka alikuwa katika nafasi ya 5 katika takwimu za wachezaji tenisi wa kike bora duniani, lakini hilo halikumfanya yeye alemae na kuona ameridhika kuwa hapo aliamini yeye ni bora na anauwezo mkubwa wa kufanya makubwa zaidi kwa nafasi yake. Alipigana kila alipopata nafasi na ndicho kilichomfanya apate mafanikio haraka ya kupanda katika nafasi za juu na kuwa mchezaji hatari zaidi kwa sasa.

Baada ya muda mfupi alifanikiwa kushika nafasi za juu ambazo zilitokana na yeye kunyanyua makombe makubwa mawili katika kipindi kifupi na ndipo dunia ikatambua uwezo wake na kuona ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi ya hayo aliyoyafanya kwenye mashindano hayo. Kiuhalisia kuwepo katika nafasi hiyo kunahitaji kujitoa sana na kujipanga vilivyo ili kusalia kwenye nafasi hiyo kwa kipindi kirefu na kudhihirisha kwamba hajabahatisha kuwa hapo hivyo jitihada zinatakuwa kwa namna yoyote.

Safari yake ya kimichezo sio ya lelemama; mwaka 2015 alikuwa nafasi ya 143 kwa takwimu za dunia nzima, mwaka 2016 alipanda hadi nafasi ya 40 na kupata tuzo kama mchezaji chipikizi wa mwaka upande wa tenisi, mwaka 2017 aliweza kushuka tena hadi nafasi ya 68 baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano mingi, 2018 aliweza kushika nafasi ya 5 kiubora duniani baada ya kuwa na kipindi kizuri sana na mwaka huu wa 2019 ameuanza vizuri baada ya kuwa mchezaji namba moja duniani kushinda michuano hiyo ya Australian Open, akitokea bara la Asia, kitu ambacho ni heshima kubwa kwake.

Acha ujumbe