Kocha wa klabu ya Interzionale Milan Simeone Inzaghi bado yupo sana ndani ya klabu hiyo vinara wa ligi kuu ya Italia kutokana na kauli aliyoitoa leo mbele ya waandishi wa habari.
Simeone Inzaghi ameweka wazi ana furaha ndani ya Inter Milan na suala la yeye kuongeza mkataba watajadili na klabu yake, Kwani ana mahusiano mazuri baina yake na viongozi wa klabu hiyo.Kocha huyo amekua akihusishwa na vilabu kadhaa ambavyo vitakua havina makocha wakuu kufikia mwishoni mwa msimu, Huku klabu ya soka ya Liverpool ndio imekua ikihusishwa zaidi na kocha huyo wa zamani wa Lazio.
Kocha huyo amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Inter Milan japo alipitia kipindi kigumu mwanzoni mwa msimu ulioisha mpaka kufikia hatua ya kuhusishwa kutimuliwa klabuni hapo lakini haikua hivo na akaendelea kufanya vizuri ndani ya timu hiyo.Klabu ya Inter Milan kwa upande wao inaelezwa wanafanya juhudi za kuhakikisha kocha Simeone Inzaghi anaongezewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na kazi nzuri ambayo anaifanya mpaka sasa.