Beki Bayern Leverkusen Bado Dili Sokoni

Beki wa klabu ya Bayern Leverkusen raia wa kimataifa wa Burkinafaso Edmond Tapsoba ameendelea kua kivutio cha vilabu mbalimbali vikubwa barani ulaya.

Beki huyo wa kimataifa wa Burkinafaso inaelezwa maskauti watatu kutoka vilabu vikubwa barani ulaya watakua wakimfatilia leo jukwaani wakati klabu yake ya Bayern Leverkusen na Borussia Dortmund wakiwa wanakipiga katika mchezo wa Bundesliga.bayern leverkusenBeki huyo aliripotiwa kufatiliwa kwa karibu na vilabu vya Manchester United na Tottenham Hotspurs kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita, Lakini kwasasa idadi ya timu kubwa zinazomtolea macho beki huyo zimeongezeka.

Beki Edmond Tapsoba amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen kwa misimu miwili mfululizo sasa, Huku akiwa moja ya wachezaji waandamizi wa kikosi hicho akifanya kazi kubwa kuhakikisha klabu hiyo inatwaa ubingwa.bayern leverkusenWakati beki Tapsoba akiwa kivutio sokoni kwa vilabu kadhaa vikubwa barabi ulaya lakini mabingwa hao soka kutoka nchini Ujerumani wanaelezwa hawana mpango wa kuachia nyota wake muhimu, Kwani wana mpango wa kushinda kwelikweli kwenye ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Acha ujumbe