Sarri: Cheslea Wanipe Mda Kuboresha Timu

Meneja wa Chelsea, maurizio sarri anasema anahitaji kupewa mda, na kuvumiliwa ili aweze kuweka mambo sawa klabuni hapo. Sarri amekuwa akiwalalamikia wachezaji wake kwa kutofuata maagizo yake wanapokuwa dimbani na matokeo yake wamekuwa wakipoteza gemu. lakini bado anasisitiza ‘Chelsea wanipe mda’ ili aweze kuboresha hali inayoendelea klabuni hapo.

Muitalia huyu alianza vyema kibarua chake wakati Chelsea wakifanya poa kwenye EPL kwa gemu takribani 18 za mwanzo. Jumatano, kikosi cha Sarrri kilipoteza gemu kwa kichapo cha bao 4-0 dhidi ya Bournemouth, kichapo ambacho kiliwaavha midomo wazi wadau mbali mbali wa soka!

Sarri anasema anataka mda wa kwenda sambamba na wachezaji na kuwafanya waelewe na kuucheza vyema aina ya mpira ambao yeye anawaelekeza. Anadai kuwa baadhi ya klabu zimekuwa na mameneja wao kwa kipindi cha miaka 5, wengine 3, wengine 2. Ameenda mbali na kuwazungumzia Barcelona akisema wameweza kujijenga kwa zaidi ya miaka 10 wakiwa wanacheza soka lao na kupata ushindi.

Sarri ambaye anaamini kibarua cha klabnuni hapo kimekuwa kigumu zadi ya alivyofikiria baada ya kujaribu kuwabadilisha wachezaji wajaribu kuendana na aina ya soka analotaka yeye walicheze. Leo anakutana na Huddesflied ambao wako mkiani kwenye ligi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.