Bosi wa Arsenal, Unai Emery amemwagia sifa meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuwa ndiye meneja bora zaidi duniani! Jumapili Arsenal anakutana na Manchester City ikiwa ni moja ya gemu ngumu kabisa kwa Washika Mitutu.
Gemu iliyopita, Arsenal walichezea kichapo cha bao 2-0 wakiwa wenyeji wa Manchester City. Emery hajasita kumwagia sifa Guardiola akisema kuwa amejaribu kuangalia timu kadhaa na hajapata kuona meneja makini zaidi kama Pep Guardiola ambaye alishaacha mataji pale Bayern Munich, Barcelona na hata hapo Manchester City.
Hii haijaenda bure, wote ni bora!
Guardiola pia amemsifia meneja huyu wa Washika Mtutu akisema kuwa ni meneja mwenye nidhamu na majukumu yake na anaamini ni meneja aliyejiandaa vyema. Bila shaka, naye atahitajhi kujiandaa vyema ili kwenda sambamba na ushindani wa gemu hii.


Gabriel
Kwel kabisa
Povel tz
Yupo vzr sana