Shirikisho la Soka nchini Mauritania FFRIM siku ya jana [jumatano] limemtangaza kocha wa zamani wa klabu ya Simba SC, Didier Gomes Da Rosa kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Da Rosa aliachia ngazi ndani ya klabu ya mwezi mmoja uliopita baada ya makubaliano ya pande zote mbili baada ya Simba SC kukubali kipigo cha magoli 3-1 na kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa Africa.
Kocha huyo mfaransa anaendelea na safari yake ya ukocha huku kwa mara ya kwanza akifundisha timu ya taifa, huku kibarua chake cha kwanza kikiwa kombe la FIFA Arab Cup linaloanza mwezi ujao.
Da Rosa pia ameungana na kocha wazamani wa viungo wa Simba SC, Adel Zrane ambaye ametangazwa kama kocha wa viungo kama pendekezo la kocha mkuu huyo.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


