Manchester United wanatarajia kuwakosa wachezaji wao 9 wakiwavaa Crystal Palace leo. Meneja wa mpito wa Man Utd, Ole Gunnar amethibitisha kwamba watawakosa baadhi ya wachezaji lakini haibadilishi lengo la timu hiyo kutaka kumaliza katika 4 bora msimu huu.
Katika wachezaji ambao wanaenda kuikosa gemu ya leo ya Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Crystal Palace ni Juan Mata, Ander Herrera na Jesse Lingard ambao walipata majeraha kwenye gemu waliyolazimisha sare na Liverpool.
Wakati Meneja huyu akitambua kuwa wana changamoto kubwa ya majeruhi, amesisitiza kuwa kila gemuambayo ipo mbele yao kwa sasa ni muhimu zaidi, ni wakati ambao Man Utd wanahitaji kucheza kama timu zaidi ili kuleta ahueni klabuni hapo.
wachezaji wengine ambaa bado wapo kwenye orodha hii ya kukosa gemu kwa ajili ya majeraha ni pamoja na Nemanja Matic, Phil Jones, Antonio Valencia, Anthony Martial na Matteo Darmian . Marcus Rashford anaweza akarejea dimbanui lakini na yeye yupo kwenye orodha hii.


Povel tz
Duh majanga