Pep Gualdiola anaamini kuwa klabu yake ipo kwenye wakati mgumu zaidi kushugulikia hali ya wachezaji klabuni hapo kufuatia shida ya majeraha. Wachezaji kama Aymeric Laporte, John Stones na Gabriel Jesus wanatarajiwa kuwa hawatakuwepo dimbani hadi baada ya lilizo ya kimataifa ya mwzi march.
Mabingwa hawa wa Ligi Kuu ya uingereza bado wapo nyuma ya Liverpool ambaye ni kinara wa ligi hiyo kwa msimu huu wakipishana kwa tofaunti ndogo kabisa ya pointi moja. Manchester City walipata ushindi mwembamba sana wa bao 1-0 dhidi ya West Ham kwa kupitia mkwaju wa penati uliowekwa nyavuni na Sergio Aguro kwenye kipindi cha pili, wakati huo wapinzani wao Liverpool wakimtandika watford bao 5-0.
City waliingia kwenye gemu wakiwa wamewakosa baadhi ya mafundi akiwemo kiungo mlinzi Ferdandinho ambaye alipata jeraha kwenye gemu waliyoshinda dhidi ya Chelsea katika fainali za Carabao Cup.
Laporte, Jesus na Fabian Delph wote walipata majeraha kwenye gemu ya hiyo. Hivyo meneja Guardiona anasema ni kipindi kigumu zaidi cha msimu kwa upande wa majeruhi.
Guardioola anaamini atawatumia vijana alionao watakaoweza kupambana katika kuelekea gemu zinazofuata ikiwemo dhidi ya Bournemouth kwenye EPL na maandalizi ya gemu za michuano mingine.

