Anthony Martial Kutua Wanda Metropolitano?

Bado kuna hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya baadhi ya wachezaji wa Man United. Anthony Martial ni miongoni mwa wachezaji hao.

Imekuwa ni kawaida kwa kila kocha anayepewa kibarua Old Trafford, atakutana na sakata lake kwenye suala la wachezaji – nani anamuuza, nani anamsajili n.k. Ilikua hivyo kwa Ole Gunnar Solskjaer na Paul Pogba na sasa, Ralf Rangnick na Anthony Martial.

Martial amekuwa akihusishwa na kuondoka United kutokana na nafasi yake kwenye kikosi cha timu hiyo kuonekana ni ndogo kadiri siku zinavyozidi kusogea. Licha ya kupewa jezi namba 9, Martial hayupo kwenye orodha ya wachezaji wanaotegemea United na sasa, ni kama mchezaji wa akiba tu.

Kocha wa Man United, Ralf Rangnick.

Kwa umri na uwezo wake uwanjani, ni ngumu kuamini Martial hana namba United na, ili kuokoa safari yake ya soka, mshambuliaji huyo anahusishwa na kuondoka United. Kocha Ralf Rangnick, amenukuliwa akisema yeye hazungumzi na wachezaji kupitia mawakala au vyombo vya habari, kama mchezaji (Martial) anataka kuondoka, akaongee nae au bodi ya wakurugenzi moja kwa moja.

Taarifa ya kuondoka kwa Anthony Martial inajaziwa nguvu na fununu za Atletico Madrid kumtaka mchezaji huyo. Inasemekana, Atletico wanaangalia uwezekano wa kumsajili Martial ifikapo Januari, 2022. Huenda kukawa na mabadilishano ya wachezaji kati ya Atletico na United kwa siku za usoni.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.