Sergio Aguero Kutoa Hotuba ya Kustaafu Soka

Nyota wa Barcelona, Sergio Aguero anatarajia kuongea na vyombo vya habari kesho juu ya hatma ya soka lake la kulipwa huku kukiwa na ripoti kuwa anataka kustaafu soka kwa sababi ya changamoto ya moyo aliyo nayo.

Nyota huyu mwenye miaka 33 hajacheza mechi yeyote tangia mwisho wa mwezi Oktoba, baada ya mechi dhidi ya Deportivo Alaves, ambapo Aguero alipelekwa hospitali akilalamika kuwa na shida ya kifua.

Kwa wakati ule, aliyekuwa meneja wa mpito Sergi Barjuan, alisema kuwa Aguero alikuwa anahisi kuwa na usingizi tu.

Sergio Aguero
Sergio Aguero

Nyota huyu alipewa angalau miezi mitatu kwa ajili ya kushughulikia hali ya afya yake, na hatua za kitabibu. Klabu pia ilidai kuwa wanafuatilia maendeleo ya afya ya Aguero kujua itachukua muda gani kuwa fiti tena.

Hata hivyo, tangia hapo taarifa zilizogonga vichwa vya habari ni kuwa staa huyu ameamua kustaafu. Kocha Xavi Hernandez alikanusha juu ya taarifa za Sergio Aguero kutaka kustaafu soka.

Taarifa za kustaafu zimerejea tena kwenye uso wa vyombo vya habari, na klabu imeweka wazi kuwa Aguero atazungumza na vyombo vya habari juu ya hatma yake hapo Jumatano.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe