Manchester City Waweka Rekodi Nyingine EPL.

 

MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baadaya ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle United jana jioni Uwanja wa St. James’ Park, Newcastle.

 

Mabao ya Manchester City yamefungwa na Ruben Dias dakika ya tano, Joao Cancelo dakika ya 27, Riyad Mahrez dakika ya 63 na Raheem Sterling dakika ya 86 huo ukiwa ushindi wa nane mfululizo na wa 34 mwaka huu.

Kocha Pep Guardiola ameiongoza Manchester City akiweka rekodi mpya ya kushinda mechi nyingi mwaka mmoja baada ya ushindi wa jana.

Manchester City wamevunja rekodi iliyowekwa na Liverpool chini ya kocha Bob Paisley kushinda mechi 33 mwaka 1982 na wanafikisha pointi 44 katika mechi ya 18 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool iliyocheza mechi 17.

Hali ni mbaya kwa Newcastle United kwani wanabaki na pointi zao 10 baada ya mechi 18 katika nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka daraja.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.