Hatimaye, Kieran Trippier amerejea Uingereza. Safari hii, atawatumikia mashabiki wa Newcastle United kule St James’ Park.
Trippier anarejea kwenye EPL akitokea Atletico Madrid ambapo alikwenda huko kupitia Tottenham Hot Spurs. Mchezaji huyu ambaye ni beki wa pembeni, anauzoefu na EPL toka wakati anachezea klabu ya Burnley.
Trippier anakwenda kuungana na Eddie Howe ambaye aliwahi kufanya nae kazi walipokuwa Burnley. Wakati ule, Howe alikuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
Dau la £12M linakamilisha usajili wa kwanza kwa wamiliki wapya wa Newcastle United na pengine, kuna uwezekano kukawa na wachezaji wengine watakaosajiliwa ndani ya dirisha hili la usajili.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


