Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Barcelona, Philippe Coutinho kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita mpaka mwisho wa msimu huu.

 

Coutinho Atua Villa Park.

 

Aston Villa wamepewa uchaguzi wa kumnunua moja kwa moja baada ya mkopo kukamilika na watalipa asilimia 50 ya mshahara wake pamoja na bonasi kipindi chote cha miezi sita atakacho kuwepo Villa Park.

Coutinho atatua Birmingham baada ya masaa 48 kukamilisha vipimo vya afya pamoja na kukamilisha utaratibu wa vibali vya kufanyia kazi nchini humo.

Coutinho na meneja wa sasa wa Villa, Steven Gerrard walicheza pamoja kwa misimu miwili na nusu wakiwa Liverpool na hiyo imechangia sababu kwa nafasi kubwa kujiunga na klabu hiyo.

Philippe alisajiliwa Barcelona akitokea Liverpool kwa rekodi ya klabu ya dau la £146m mwezi January mwaka 2018 lakini alishindwa kufanya vizuri Camp Nou kutokana na majeraha.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa