Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ameelezea kwa nini timu yake ilikuwa haina namna zaidi ya kuomba kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya Arsenal wiki iliyopata kwenye fainali ya kwanza ya Carabao Cup iliyopangwa kupigwa kwenye dimba la Emirates.
Uwanja wa mazoezi AXA Training Centre ililazimika kufungwa kwa siku kadhaa, na kocha msaidizi Peter Krawietz ndie aliekuwa anaongoza maandalizi ya mchezo wa jumapili dhidi ya Shrewsbury Town kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu wa kombe la FA Cup, huku Klopp na Pep Lijnders wakiwa wamejitenga kutokana na maambukizi ya Uviko-19.

Jurgen Klopp ameelezea taratibu zilizofanywa mchezo wao kuahirishwa na kumfanya kutoweza kuchagua wachezaji kwa haraka kwenye kikosi cha timu ya wakubwa, “matokeo ya uongo ni matokeo ya vipimo unayopat.
“Unapata matokeo sahihi baada ya kuweza kufanya kipimo tena, siku moja au siku moja na nusu baadae unapata matokeo yanayofanana na uhalisia.
“Haibadili kitu chochote kwa kujitenga au vyovyote. Lakini kuthibitisha lipi kosa lipi sio kosa sababu unataka kujua na unahitaji kujua inabidi ufanye kipimo kwa mara tatu na matokeo ya kipimo cha tatu yanakuonyesha majibu sahihi.
“kati ya kipimo cha kwanza na kipimo cha pili, kipimo cha pili na cha tatu, huwezi kutumia wachezaji, hizo ndo sheria na sheria ni sheria za wote.” Alisema Klopp
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

