Arteta amemjibu Mourinho ambaye aliwasiliana na kiungo Granit Xhaka na kumtaka kupata chanjo ya uviko 19.
Mkufunzi huyo wa timu ya Roma ambaye aliwasiliana na Xhaka kupitia mtandao wa Instagram na kumtaka apate chanjo, baada ya kupima na kukutwa na maambukizi ya uviko-19.
Chama cha soka cha Uswisi kilitoa taarifa kuwa, Xhaka alikataa kupata chanjo na alipopimwa ndipo akagundulika kuwa na maambukizi na imepelekea kukosa mechi za kimataifa ambazo Uswisi imecheza, mechi ya kirafiki dhidi ya Ugiriki na mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Italia na Ireland ya Kaskazini waliyotoa sare.

Arteta ameuliza kama Mourinho ana haki ya kuhamasisha wachezaji kupata chanjo, japo yeye mwenyenye anasema, maamuzi ya wachezaji yanapaswa kuheshimiwa.
Mourinho ambaye alijunga na Roma majira ya kiangazi alijaribu kumsajili Xhaka kama usajili wake wa kwanza mara tu alipopewa kandarasi na Roma.
Arsenal imepoteza mechi zake tatu za mwanzoni na wanajiandaa kukutana na Norwich City jumamosi hii.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.



[email protected]
Nice update