Pigeni Kelele Lakini Kosi la Gamondi Halibadiliki

gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga Muargentina, Miguel Gamondi hataki masikhara amepanga kuendelea kikosi alichokuwa anakitumia katika hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, katika Ligi Kuu Bara kwa kuanzia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga inatarajiwa kuvaana dhidi hya Mtibwa Sugar Jumamosi hii saa 12:30 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Bashiri mechi hii na nyingine za Wikiendi hii upate maokoto ya MERIDIANBET kwenye Jamvi lako.

Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani wakiwa na hasira ya kupata matokeo mazuri, ili warejeshe morali ya kufanya vema katika mchezo wa marudiano wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Medeama SC.

Gamondi alisema kuwa alianza maandalizi ya mchezo huo tangu juzi Jumanne asubuhi baada ya mapumziko ya siku moja baada ya kutoka kucheza dhidi ya Medeama. MERIDIANBET kila mechi ni ushindi tu, usiogope kubeti timu yeyote ina pesa yako sasa.

Gamondi alisema kuwa wataingia uwanjani bila ya kuwadharau Mtibwa Sugar, badala yake atatumia kikosi alichoendelea kukitumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kilichotoka sare dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri na Medeama ya Ghana.

Aliongeza kuwa kikubwa anataka kuona timu yake, ikiendelea na ushindi mkubwa wa mabao ili warejee kileleni katika ligi, hilo linawezekana kwao kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.

“Tunaendelea vizuri na kambi yetu Avic Town, Kigamboni kikubwa tunataka kuona tukirejea katika ligi, tukiwa imara baada ya kutoka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu, ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo, tunafahamu Mtibwa Sugar mwenendo wao mbaya katika ligi, lakini hiyo haitufanyi tuingie kwa kujiamini.

“Kikosi changu hakitakuwa na mabadiliko, nimepanga kutumia kikosi nilichokuwa nakitumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kutokana umuhimu wa mchezo na mengine ya ligi inayofuatia,” alisema Gamondi.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe