IPO wazi kuwa mtambo wa kazi uliotambulishwa ndani ya Yanga ni noma kutokana na majukumu yake kuwarahisishia kazi benchi la ufundi la timu hiyo. Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameongezewa mtu mwingine wa kazi kwaajili ya kuongeza nguvu kwenye kusaka ushindi.
Ni Mpho Maruping kutoka Afrika Kusini ambaye Desemba 14 alitambulishwa rasmi kuwa ni Mtaalamu wa Kusoma Video za Wapinzani (Video Analyst) wa kikosi hicho. Weka utabiri wako MERIDIANBET na uibuke mshindi kwenye mechi mbalimbali za LIGI KUU YA NBC na kote duniani.
Mpho amewahi kuwa mchezaji katika vilabu mbalimbali vya ligi kuu nchini humo na kabla ya kutimkia Yanga alikuwa akihudumu kama Mtaalamu wa Kusoma Video za wapinzani kwa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) iliyofanikiwa kuchukua Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON 2022) na ile iliyofika 16 Bora ya Kombe la Dunia kwa Wanawake 2023 nchini Australia. Meridianbet wanaotoa odds kubwa kwenye mechi zote kila siku, ni wewe tu kuweka utabiri wako.
Hivyo kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni pamoja na mchezo ujao dhidi ya Medeama kazi yake kubwa itakuwa ni kushirikiana na benchi la ufundi kujadili ubora na udhaifu wa wapinzani wao. Kwa odds kubwa na machaguo kibao unajiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda MERIDIANBET. BASHIRI HAPA.