Ladack Chasambi Anaenda Zake Simba SC

chasambi simba

INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba umemalizana na winga wa mabao ndani ya Mtibwa Sugar, Ladack Chasambi. Kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana uwezo wa kucheza winga pamoja na nafasi ya kiungo mshambuliaji. Meridianbet moja kati ya machimbo ya utajiri kwa watu wanaobashiri kwenye maduka ya ubashiri.

Nyota huyo jina lake lipo pia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambacho kilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi za kimataifa hivi karibuni. Ilikuwa ni kwenye kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo kiungo huyo alijumuishwa katika kupeperusha bendera ya Tanzania.

 

Miongoni mwa timu ambazo kazifunga ndani ya Ligi Kuu Bara ni pamoja na Geita Gold. Moja kati ya Sababu zilizowavutia Simba ni uwezo wa kijana huyo katika kushambulia na kukaba. Kuwa mmoja kati ya washindi wa kila siku unapobeti na MERIDIANBET kwa Odds Kubwa. BASHIRI HAPA.

Habari zinaeleza kuwa tayari nyota huyo mwenye pasi tatu za mabao ndani ya ligi Kuu ya NBC amefikia makubaliano mazuri na Simba.

Ikiwa dili lake litajibu huenda katika dirisha dogo akatambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kuanza majukumu yake mapya kwa msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa Simba.

Acha ujumbe