Kiungo wa klabu ya Simba raia wa Naijeria Vicent Akpan aliesajiliwa kutoka Coastal Union ya mkoani Tanga maarufu kama wanamangushi imeelezwa kua atasalia ndani ya msimbazi.

msimbazi, Akpan Kusalia Msimbazi., Meridianbet

Kiungo huyo aliesajiliwa mara tu baada ya kumalizika kwa ligi ya Tanzania Bara maarufu kama NBC premier league mwanzo ilisemekana ana uwezekano mkubwa wa kutolewa kwa mkopo baada ya mwalimu Zoran Maki kutoridhishwa na uwezo wake aliounesha katika michezo kadhaa.

Mwalimu Zoran ameeleza atatumia michezo mitatu ya kirafiki inayokuja hapo mbele kumpima mchezaji huyo ili aweze kusalia katika viunga vya Msimbazi. Klabu ya simba inatarajiwa kucheza michezo yake mitatu siku kadhaa mbele ambayo ndo ambayo itatumika kama kipimo cha mwisho cha kiungo huyo kinanaijeria.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa