Chelsea walikuwa na ofa ya awali ya takriban paundi £40m-£45m iliyokataliwa na Everton mapema mwezi huu lakini klabu hiyo iko tayari kuongeza ofa yao hadi paundi milioni 60 ili kufanikisha kumpata Anthony Gordon msimu huu wa joto.

chelsea, Chelsea watoa Paundi £ 60M kumsajili Anthony Gordon., Meridianbet

Mawasiliano baina ya pande hizo mbili yanaendelea na Chelsea wapo tayari kuongeza ofa yao hadi kiashi hicho walichokitaja kuwa watatoa. Mkataba unabaki mezani kwa Gordon kukubali kwenda Chelsea au vinginevyo ambapo kwa sasa ana mkataba na Everton hadi mwaka 2025.

Frank Lampard anahitaji kuongeza mshambuliaji mmoja kwenye kikosi chake kabla ya dirisha kufungwa, hivyo anategemea mpango wa usajili wa Gordon ukamilike ili apate pesa za kutimiza mipango yake.

chelsea, Chelsea watoa Paundi £ 60M kumsajili Anthony Gordon., Meridianbet

Tottenham walitaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kwa mkataba wa mabadilishano na Richarlison kwa jumla ya £80m mapema msimu wa joto lakini hawakufanikiwa. Newcastle pia ilifanya mbinu, lakini haikuwasilisha ombi rasmi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa